Powered by Blogger.

Nay wa Mitego kuachia video ya Pale Kati iliyofungiwa,fahamu zaidi hapa..


Baada ya kutangaza kufungiwa na BASATA,msanii wa rap nchini Nay wa Mitego amedai kuwa ameshamalizana na baraza hilo kwa kufuta taratibu zilizoweka na sasa yupo huru kuendelea na kazi zake za kisanii ambapo anatarajia kuachia video ya Pale Kati Patamu.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa radio,Nay amesema kwamba wimbo huo una video nne,na ataanza kutoa video ya kwanza ndani ya juma hili na kudai video hiyo imefanywa kwa wimbo wa Pale Kati original ambao ulifungiwa na kueleza kuwa hatoutolea hapa Tanzania.
Video zipo nne na zipo tofauti, lakini mpaka sasa orijino ‘version’ ya ‘Pale kati’ inachezwa sana nje ya nchi, kwani ina nguvu kubwa sana nje ya nchi, mfano kama Kenya, Uganda, Ghana, Afrika Kusini, Nigeria, yaani kazi haina video lakini inafanya vizuri, hivyo tutaachia video ambayo ‘Audio’ yake ni ile iliyofungiwa hapa nyumbani ingawa video hii tutaachia nje ya Tanzania” alisema Nay wa Mitego
Source:EATV
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment